Nyota Yetu
07.05.2011
Deborah Mwenda
Nyota Yetu: DEBORA MWENDA
Nyota yetu wiki hii ni mwanahabari mkongwe wa Radio Tanzania, mama Deborah Mwenda., yeye amepokea tuzo mbalimbali na nishani kutokana na utendaji bora hasa katika masuala ya watoto.
Deborah Mwenda amesoma katika shule ya msingi Mvumi Dodoma, alijiunga na sekondari ya wasichana Tabora na kuhitimu kidato cha nne, amehudhuria kozi zaidi ya kumi za uandaaji na uendeshaji wa vipindi kutoka nchi kadhaa kama Uholanzi, Marekani, Uingereza, Misri na Namibia. Anapenda kukaa na watoto, kusoma vitabu vya riwaya na ana kipaji cha uigizaji.
Hapo nyuma kidogo gazeti la Mwananchi lilikutana naye katika shule yake iliyoko Kunduchi, jijini Dar es Salaam, nakufanya mazungumzo naye, na haya ndiyo Yalikuwa mahojiano yao.
SWALI:Uliwahi kuwa na ndoto zozote za kuwa mwanahabari hapo kabla?
JIBU: Sikuwahi kuwa na ndoto hizi kwa sababu ilikuwa ni taaluma mpya na hata vyombo vya habari vilikuwa vichache.
JIBU: Sikuwahi kuwa na ndoto hizi kwa sababu ilikuwa ni taaluma mpya na hata vyombo vya habari vilikuwa vichache.
SWALI: Ilikuwaje ukawa mwanahabari mahiri sasa?
JIBU: Wakati ule ajira zilikuwa nyingi na wasomi walikuwa wachache, hivyo maofisa kutoka serikalini walikuwa wakija shuleni kunadi aina za kazi ili tukimaliza shule twende kuzifanya. Siku moja mzungu alikuja akasifia kazi nyingi na moja wapo ilikuwa utangazaji wa habari.
Nilijikuta navutiwa na kazi hiyo na nilipomaliza kidato cha nne nilikwenda Radio Tanzania nikamkuta mzungu mmoja mwanamke ambaye alinipa kifungu cha habari nisome, nilipomaliza aliniambia uanahabari siuwezi nikatafute kitu kingine.
Hata hivyo mzungu yule aliniona kuwa nina kipaji kingine, siku moja niliitwa nikacheze tamthiliya ambayo iliitwa “Miembeni kwa akida”, nilifanya vizuri katika kuigiza na nilikuwa sisiti kukumbushia suala la utangazaji, ndipo siku moja nilipobahatika kujaribu kutangaza na nikaweza.

SWALI: Wewe ni miongoni mwa wanahabari wakongwe je, ni nini siri ya mafanikio yako?
JIBU: Nilikuwa nafanya kazi kwa kujituma na kila nilichoagizwa na bosi wangu sikusita kufanya, nilipita karibu idara zote za utangazaji kama idhaa ya taifa, elimu, biashara hata uhusiano wa kimataifa.
Lakini pia nilikuwa mbunifu. Mimi ndiye niliyebuni kipindi cha “Mama na Mwana”. Mwaka 1970 ulikuwa ni mwaka wa watoto, bosi wangu aliniuliza tufanye kitu gani kuhusu siku hiyo, ndipo nilipokuja na wazo hili.

SWALI: Changamoto gani ulikutana nazo ulipokuwa mtangazaji
JIBU: Wanawake hawakupewa nafasi za juu za uongozi katika vyombo vya habari kutokana na kasumba, lakini sisi wenyewe tulikuwa hatujiamini. Changamoto nyingine ilikuwa pindi tupewapo majukumu ya nje, kama umepangwa na mwanaume basi yeye atajiona ndiyo kiongozi wako, atataka akutawale hata kukugombeza ikiwezekana.
SWALI: Mafanikio yapi umeyapata kupitia taaluma hii?
JIBU: Kwanza kusoma nchi mbalimbali, kujuana na watu ambao walinijenga kimawazo, lakini kubwa hasa ni baada ya kustaafu mwaka 1995 niliweza kuanzisha shule ya Chekechekea na baadaye Msingi, inaitwa Bahari Primary School, inafundisha kwa lugha ya Kiingereza ni ya bweni na kutwa.
SWALI: Unawashauri nini wanahabari wa sasa?
JIBU: Wawe makini wasiifanyie taaluma hii mzaha au kimbilio la wakosa kazi.

SWALI: Unamshukuru nani kwa mafanikio yako?
JIBU: Mume wangu John Mwenda aliyenipa moyo na kunisaidia kuanzisha shule, watoto wangu wanaonipa mawazo na misaada mbalimbali.
JIBU: Mume wangu John Mwenda aliyenipa moyo na kunisaidia kuanzisha shule, watoto wangu wanaonipa mawazo na misaada mbalimbali.
04.30.2011
Musa Njechele
Nyota Yetu.
Nyota Yetu.
Katika Nyota yetu leo wanatemino tunamtunuku MUSA NJECHELE: shujaa mwenye ulemavu wa kutokuona, lakini ni fundi mahiri wa simu.
Musa anamiliki ofisi ya duka na ufundi wa simu lililoko eneo la Yombo Kilakala maarufu kwa jina la Chedi au Sharp Corner lililopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Ofisini kwake hapo utakutana na watu wanaopishana kuingia kwa lengo la kujipatia ama huduma ya kupiga simu, kununua vocha au kutengenezewa simu.
Alipoulizwa Musa anasema kuwa amefanya kazi hiyo kwa miaka saba tu, na alianza ufundi wa simu mwaka 2003, baada ya kufanikiwa kumiliki kwa mara ya kwanza simu ya mkononi.
Njechele ambaye kitaaluma ni mwalimu, anasema alipoanza biashara ya simu mwaka 2003 alikuwa anafanyia kazi katika mazingira duni kwenye kibanda cha mbao, baada ya miezi saba akahamia kwenye kontena la mabati lenye ukubwa wa futi nane kwa saba, na Agosti mwaka jana aliweza kupangisha fremu iliyojengwa kwa tofali na bati sehemu anayofanyia biashara zake hadi leo. Anasema kazi hiyo imemuwezesha kuongeza pato la familia yake pamoja na kutoa nafasi za ajira isiyo rasmi kwa vijana watano kwa nyakati tofauti.

Je, alianza vipi kufanya na kuvutiwa na shughuli hii? Njechele anasema kuwa ndoto yake ilianza mwaka 2003 baada ya kufanikiwa kununua na kumiliki simu aina ya Sony Ericsson 1018. Kwa kuwa alikuwa na shauku ya kuona muundo wa simu, alidhamiria kuwa fundi simu jambo ambalo lilimpa msukumo wa kuifungua simu yake na kudadisi ilivyotengenezwa.
“Mwaka 2003 ndipo nilianza kazi ya kutengeneza simu...kwa kuwa sikuwa na uwezo wa kuona niliwasiliana na mafundi wengine na kunipa maelezo ya vifaa vilivyo ndani ya siku,” anafahamisha.
Anasema ilikuwa vigumu watu kumuamini hivyo alianza kwa kuuza vocha za simu, kurekebisha tarehe na saa na kuweka nyimbo kwenye simu.
“Biashara ni uthubutu...ingawa sikuwa na uwezo wa kuona niliweza kurekebisha simu mpya kwa kuchagua lugha, mfumo wa kutuma ujumbe mfupi, tarehe na muda jambo ambalo liliwezesha watu kujenga imani na mimi,” anaeleza.
Baada ya muda mfupi aliweza kutengeneza simu zilizoharibika na hivi sasa ameweza kupanua huduma hiyo na kuajiri vijana wawili.

Hata hivyo kazi hiyo ni ya ziada. Njechele bado ni Mwalimu katika Shule ya Msingi Sandali na anafundisha masomo ya Sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Anasema ingawa wanafunzi hawana kompyuta za kujifunza kwa vitendo, Njechele anasema wana uwezo wa kufuatilia vyema masomo ya nadharia.
Yeye ana uwezo wa kutumia kompyuta kwa kutumia programu maalumu zinazowasaidia wasioona kama vile programu ya Dolphin, Narrator na Screen wonder. Anasema ndoto zake za baadaye ni kumiliki duka kubwa la simu pamoja na kufundisha vijana jinsi ya kutumia teknolojia ya kisasa.
Anaomba jamii isiwatenge watu wenye ulemavu, bali iwasaidie wenye uthubutu wa kujituma na kuhamasisha wale wasiokuwa na uthubutu ili kuondoa dhana kuwa wenye ulemavu hawawezi kufanyakazi na kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Huyo ndiye Musa Zuberi Njechele, mlemavu asiyeona aliyethubutu kufanya mambo makubwa licha ya hali aliyonayo. Kwa hakika, ni mfano wa kuigwa na nyota wa kweli katika jamii hii iliyozungukwa na vijana wengi wanaoshinda vijiweni kwa kisingizio cha kukosa ajira.

Chanzo: Habari Leo
Abdallah Nyangilo
04.23.2011Leo wanatemino tunamtunuku Abdallah Nyangalio: fundi stadi wa nguo asiyeona.
Abdallah ni miongoni mwa watu wenye ujasiri na uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto za maisha. Ni jasiri kwa sababu ameweza kupambana na ulemavu wa macho alioupata ukubwani, na kuhakikisha anajitafutia maisha kwa njia halali. Yeye kwa sasa ni miongoni mwa mafundi hodari wanaokubalika ndani na nje ya nchini. Je, ilikuwaje hata akawa katika hali ya ulemavu aliyonayo sasa?
Nyangalio alipohitimu shule alifanya biashara kwa lengo la kutafuta mtaji kumuwezesha kutimiza ndoto za kuondokana na umasikini, lakini aliugua na kupofuka macho hivyo kujikuta katika kundi la watu wenye ulemavu. Kupofuka kwake kulikuwa mtihani mkubwa sana, lakini hakukata tamaa ya maisha, bali alikuwa mwepesi kukubali kuishi katika hali iliyomkuta, kisha kutafuta mbinu zitakazomuwezesha kujipatia kipato ili kuepuka kuishi maisha tegemezi.
Uwezo wake wa kukabiliana na changamoto za maisha ndio uliomfanya Nyangalio kuwa fundi stadi wa nguo na habari zake zimeweza kusambaa sehemu mbalimbali Afrika Mashariki na Kati kama kielelezo kwamba ulemavu sio mwisho wa maisha.
Mnamo mwaka 1988 ,Abdalah alipata maumivu makali ya kichwa yaliyoambatana na kukosa usingizi, hali hiyo ilisababisha aende katika hospitali mbalimbali kutafuta tiba bila mafanikio. Baada ya kufanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Muhimbili, Nyangalio aliambiwa kuwa tatizo la kukosa usingizi linatokana na hitilafu iliyojitokeza katika mishipa ya macho na tiba pekee ni upasuaji utakaomfanya kuwa kipofu kwa maisha yake yote.
Abdalah anakiri kuwa ilikuwa vigumu kukubaliana na hali hiyo kwa sababu alishindwa kutambua mchana na usiku kutokana na kiza kinene kilichotanda kwenye macho yake. Alihofia kuishi maisha tegemezi. Hata hivyo daktari aliyemfanyia upasuaji alimfariji na kumpa nafasi ya kukaa katika hospitali ya Muhimbili kwa miezi mitatu akipewa ushauri pamoja na mbinu za kuishi katika hali ya kutoona. Anasema mbinu hizo alizojifunza ni pamoja na elimu juu ya maisha na changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu na jinsi ya kupambana nazo,
Pia alifundishwa kusoma maandishi maalumu kwa watu wasioona, kutumia cherehani pia jinsi ya kukata na kushona nguo mbalimbali.
Baada ya kutoka hospitalini, alikutana na changamoto nyingi katika maisha kwa kuwa baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki walimuona kama mzigo hivyo baadhi ya ndugu walilumbana wakitupiana jukumu la kumtunza.
Anasema pamoja visa na mikasa iliyompata aliweka mikakati ya kushinda changamoto katika maisha ili aweze kuudhihirishia ulimwengu kuwa binadamu ameumbwa ili aweze kukabiliana na taabu mbalimbali kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu. Aliendelea kumuamini na kumtegemea Mungu kwa kila jambo alilolifanya huku akiwa na matumaini makubwa kuwa Mungu atampa njia nyingine ya kuishi bila ya kuwa tegemezi.
Baada ya miezi saba ya ugonjwa alirudi katika shughuli za biashara ndogo ndogo kwa kuuza nguo za mitumba pamoja na kushona nguo kwa kutumia cherehani ya jirani yake. Alidunduliza mtaji mpaka alipopata uwezo wa kununua cherehani yake na kuanza kazi ya kushona nguo mbalimbali hasa sare za wanafunzi wa shule ya msingi. Pia alijiimarisha kiuchumi na kurudia maisha ya kujitegemea kama kiongozi wa kaya.
Kipaji cha Nyangalio alianza kufahamika mwaka 1994 wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu wa macho maarufu kama siku ya Fimbo Nyeupe Duniani.
“Wakati wa maadhimisho hayo mgeni rasmi alisifia suti aliyokuwa amevaa aliyekuwa kiongozi wa taasisi ya wasioona. Kisha akaambiwa kuwa suti hiyo ilishonwa na fundi asiyeona hivyo nikaanza kujulikana kuanzia siku hiyo,” anasema Nyangalio anayekumbuka kuwashonea nguo Anna Abdallah, wakati huo akiwa Waziri wa Afya, Sophia Simba, Joel Bendera na wengine wengi.
Hivi sasa Nyangalio anafanyia shughuli zake Mbagala Kibonde Maji jijini Dar es Salaam ambako amejenga makazi yake ya kudumu, amefanikiwa kusajili kampuni inayojulikana kama Nyangalio Fashion Centre ambayo ana mpango wa kuitumia kutoa elimu ya ufundi cherehani hususani kwa watu wasioona.
Nyangalio amewahi kutoa elimu ya ushonaji kwa watu wenye ulemavu ambayo yalifadhiliwa na Taasisi ya Taifa ya Huduma ya Maendeleo ya Wasioona (TNIB), ambapo wanafunzi wanne walihitimu na kufaulu kwa kiwango cha kuridhisha.
Hivi sasa ana mashine mbili za kushonea ambazo anategemea kuzitumia kutoa mafunzo. Anaomba watu wenye uwezo kumsaidia ili kupata wafadhili wa kutimiza ndoto zake za kuanzisha shule ya ushonaji hususani kwa watu wenye ulemavu.
Ustadi wa Nyangalio umemuwezesha kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya ujasiriamali yaliyofanyika nchini pia katika nchi za Zambia na Kenya. Huyo ndiye Abdallah Nyangalio ambaye hakukata tamaa baada ya kupata ulemavu, bali aligeuka kuwa jasiri kiasi cha sasa kuwa mmoja wa watu wa kuiga mfano.
1, 2011 - Dr. Asha-Rose Mtengeti Migiro
Leo tunaanza mwaka kwa kumtunuku Dr. Asha-Rose Mtengeti Migiro kama Nyota yetu wiki hii. Maana yeye ametuonyesha dhahiri kwamba mafanikio ya Mtanzania yapo kona zote kitaifa na kimataifa pia.
Februari mwaka 2007 ni tarehe ambayo Dr. Asha-Rose Mtengeti Migiro hawezi kuisahau kirahisi. Hii ndiyo siku alipokabidhiwa rasmi ofisi na majukumu ya unaibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa cheo ambacho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997 kilikuwa hakijawahi kushikiliwa na sio tu na mwanamke yeyote mweusi bali pia mwafrika yeyote.
Dr.Asha-Rose Migiro ndiye mwanamke wa kwanza mweusi kushikilia wadhifa huo na pia mwafrika wa kwanza. Mwanamke mwingine ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kushikilia cheo hicho alikuwa ni mzungu raia wa Canada Louise Frechette ambaye alianza kukitumikia cheo hicho mapema mwaka 1998.
Dr.Migiro anayo historia nyingine ya kujivunia. Yeye ndio alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania tangu nchi yetu ilipopata uhuru mwaka 1961. Aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje mwaka 2006.
Hivi leo Dr.Asha Rose Migiro ambaye ni mke wa Professa Cleophas Migiro na pia mama wa watoto wawili wote wakiwa wakike, ni fahari ya Tanzania. Ndiye “balozi” wa Tanzania anayetambulika kirahisi zaidi kimataifa hivi sasa.
Yeye mwenyewe, katika mahojiano mbalimbali aliyofanya na vyombo vya habari kufuatia uteuzi wake, anasema uteuzi ule ulimshangaza lakini pia aliuona uteuzi wake kama sifa kwa bara zima la Afrika. Waliowahi kufanya naye kazi wanasema hawakushangaa kusikia kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon amemchagua Dr.Migiro kwa sababu ni mchapakazi, mnyenyekevu na msomi aliyebobea katika masuala ya sheria. Unyenyekevu, utu na uungwana ni sifa zingine ambazo zinafanya majumlisho ya siri ya mafanikio yake.
Lakini Dr.Asha- Rose Migiro ametokea wapi? Historia yake inaonyesha kwamba alizaliwa Songea, Kusini mwa Tanzania mnamo tarehe 9 Julai mwaka 1956. Wazazi wake ni wenyeji wa mkoani Kilimanjaro ambako ndipo ilipo asili yake. Kikabila ni mpare.
Alianzia elimu yake ya shule ya msingi katika shule ya msingi Mnazi Mmoja iliyopo jijini Dar-es-salaam mwaka 1963 mahali ambapo aliposoma mpaka mwaka 1966 alipohamia shule ya msingi Korogwe iliyopo Korogwe,Tanga kuanzia mwaka 1967 hadi 1969 alipomalizia elimu yake ya msingi. Kuanzia mwaka 1970 hadi 1973 hapo alijiunga na shule ya sekondari ya wasichana WeruWeru iliyopo Moshi,Kilimanjaro. Kwa elimu ya high school Dr.Migiro kuanzia mwaka 1974, alisomea katika shule ya Sekondari ya Korogwe iliyopo Korogwe,Tanga ambapo alihitimu mwaka 1975.
Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam mwaka 1977 kuchukua shahada ya kwanza ya sheria. Alihitimu mwaka 1980. Baada ya hapo alifanya kazi ya uwakili kwa muda mfupi. Kuanzia mwaka 1982 hadi 1984 Dr. Migiro alirejea tena katika Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kwa ajili ya shahada ya pili ya Sheria (Masters).
Safari ya kimasomo ya Dr. Asha-Rose Migiro haikuishia hapo kwani mwaka 1988 alijiunga na Chuo Kikuu cha Konstanz kilichoko nchini Ujerumani kwa ajili ya masomo ya kutoka chuo hicho hicho kikuu cha Dar-es-salaam mnamo mwaka 1984. Baada ya hapo alikwenda nchini Ujerumani kusomea shahada ya udaktari wa falsafa (PhD) katika masuala hayo hayo ya sheria katika Chuo Kikuu cha Konstanz ambapo alihitimu masomo yake mwaka 1992.
Kabla ya kuelekea Ujerumani, kikazi tayari alikuwa ni mwajiriwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa mkufunzi msaidizi mwaka kuanzia mwaka 1981 na baadaye, baada ya kurejea toka masomoni Ujerumani, kupanda katika ngazi za mhadhiri msaidizi, mhadhiri hadi mhadhiri mwandamizi, cheo alichokuwa nacho mpaka mwaka 2000 alipoingia kwenye siasa. Aliingia kwenye siasa na moja kwa moja kugombea ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa taasisi za elimu ya juu.
Baada ya kumalizika kwa uchaguzi, aliteuliwa na Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, nafasi aliyoishika hadi mwaka 2005. Huyo ndio Dr.Asha-Rose Migiro, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, umoja ulioanzishwa mnano mwaka 1945 na wenye makao yake makuu New York nchini Marekani.
Mama Asha Rose Migiro,
Wewe ni fahari yetu, na sisi tunajivunia!
Januari 8, 2011 - John Stephen Akhwari
Leo tunamtunuku John Stephen Akhwari. Nyota hii imengara ndani na nje ya nchi kwa sababu ambayo wengi wetu tusigedhani ingeweza tokea.Yeye hufahamika kama alama ya Ushujaa duniani kote na historia yake imetumika kujenga na kuwatia moyo wanamichezo wengi kimataifa waweze kufikia ushindi.
Bwn. Akhwari yeye ni Mzawa halisi wa Tanzania. Mnamo mwaka 1968 katika Michezo ya Olimpiki ya mji wa Mexico, alikuwa miongoni mwa ujumbe wawatanzania walioshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki kwa mara ya kwanza mara baada tu ya nchi yetu kupata uhuru na alikuwa na matarajio makubwa ya kupata medali kwenye michezo hiyo kwani kabla ya kushiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Mexico , Bw. Akhwari alipata nafasi ya kwanza ya mashindano ya Marathon ya Afrika ya Mashariki na nafasi ya kwanza ya mashindano ya Marathon ya Afrika ya Kusini.
Walipofika mji wa Mexico, wanamichezo wa Tanzania waliona tofauti kubwa ya kijiografia kati ya Mexico na Tanzania. Mexico ni mji ulioko kwenye mwinuko wa juu kutoka usawa wa bahari, na kabla ya kwenda huko wawakilishi hawa wa Tanzania walifanya mazoezi mengi kwenye ukanda wa bahari Dar es salaam lakini kufuatia na tofauti kubwa ya kijiografia mashindano haya yaliwapatia changamoto kubwa sana.
Wakati wa siku ya shindano lenyewe bwana Stephen Akhwari wakati akikimbia alishindwa kuhema vizuri, alishikwa na misuli na pia alianguka na kupata majeraha mengi sana ambayo yalimuumiza goti lake vibaya katika mbio hizo za kimataifa.
Wengi wetu tungepatikana katika hali hii iliyompata Stephen tungekuwa na sababu lukuki za kutoendelea. Kwake Stephen kukata tama ilikuwa ni starehe ambayo gharama yake hakuweza kuilipa. Kwa michubuko na maumivu mengi aliyozidi kuyapata huku misuli ikiendelea kumkaza aliendelea kukimbia na hata pale wahudumu wa huduma ya kwanza walipomfuata na kumuomba aache kukimbia kwa sababu angeweza kudhuru afya yake alikataa na kuendelea na mbio hizo.
Ilikuwa kama mida ya jioni sana na ambapo washindi wa kwanza kukanyaga utepe wa kumaliza mbio hizo walikuwa wameshawasili uwanjani hapo saa moja lililopita na watu walikuwa wameshaanza kuondoka uwanjani; waliobaki walikuwa ni waandishi wa habari wachache na washangiliaji waliokuwa wakijifungasha kuelekea makwao.
Ghafla zikaanza sikika sauti za vingora vya polisi ambavyo ni jadi kuwasindikiza wanariadha wote wanaoshiriki mbio mpaka mwisho wao na taratibu zikaanza sikika sauti ya makofi kutoka kwa mmoja hadi mwingine kwa wale waliokuwapo uwanjani. Wengi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo hawakuamini kile walichokuwa wanakiona.
Kwa mbali alionekana bwana Akwhari akiwa na jezi zilizobeba bendera ya Tanzania akikimbia peke yake kwa kuchechemea huku mguu wake umezungukwa na bandeji na uso wake kuonekana na maumivu mengi. Shwange za mishangao zilizidi kutanda uwanjani hapo kila mtu akimtia motisha Stephen ili aweze kumaliza mbio zile.
"Wachezaji 63 miongoni mwa 80 walikuwa hawakuweza kumaliza mashindano, lakini mimi nilishikilia mpaka mwisho, kwani nilivumilia mpaka nikaingia uwanja wa michezo, ingawa ni wa mwisho." Anasema bwana Akwhari.
Alipoulizwa na waandishi wa habari kwanini aliendelea kukimbia wakati watu wote walimaliza kipindi kirefu kabla yake na pia kwa kuwa alikuwa na maumivu mengi alijibu, ‘Nchi yangu haikunituma maili 5,000 kuja mji huu wa Mexico kuanza mbio, bali nchi yangi imenituma kuja kumaliza mbio’ , yaani; "My country did not send me to 5,000 miles to Mexico City to start the race. They sent me 5,000 miles to finish the race."
Mashindano haya yalimpatia cheo na kumuita mfalme bila taji - "a King without crown." Na baada ya hapo maneno yake yanakumbukwa kwenye historia ya Michezo ya Olimpiki. Na baada ya mashindano hayo, Bw. Akhwari pia alishiriki kwenye mashindano mengi ya kimataifa ya Marathon, na kupata mafanikio.
Mwaka 1983, Tanzania ilimpa Bw. Akhwari medali ya "Shujaa wa taifa" kutokana na mchango mkubwa alioutoa katika shughuli za michezo za Tanzania. Stephen ameandikwa kwenye vyombo vya habari mbalimbali kimataifa na pia huko Uchina kuna wimbo unaitwa ‘shujaa’ umeimbwa kwa ajili yake.
Pia ameazimisha jina lake kwa John Stephen Akhwari Athletic Foundation, Asasi ambayo inasaidia watanzania kwa mafunzo ya michezo ya Olympiki. Mwaka 2000 kwa heshima ya jina lake na kile alichokifanya kihistoria katika ulingo wa michezo kitaifa alialikwa Sydney, Australia na baadae alialikwa Beijing, Uchina kama balozi wa ukarimu katika maandalizi ya michezo ya olyimpic 2008. Kwakweli, historia yake ni urithi ambao sisi sote tunapaswa kujifunza kutoka kwake.
John Stephen Akhwari,
Wewe ni Nyota yetu na sisi tunajivunia!
Januari 15, 2011 - Edward Moringe Sokoine
Edward Moringe Sokoine,
Januari 22, 2011
Katika Nyota yetu leo tunamtunuku Edward Moringe Sokoine . Yeye ni miongoni mwa wanasiasa bora na adimu sana hapa nchini. Yeye alionyesha njia ya kweli ya uongozi kwa kiwango cha kutia motisha ya kutosha ya kwamba, uongozi bora unaojali wananchi ni halisia na unaweza fanyika katika kizazi chetu hiki. Yeye alikuwa ni mwanasiasa halisi nchini, na pia lifanyika Waziri Mkuu kwa mara mbili, kwaza 13 Februari, 1977 hadi 7 Novemba, 1980, na tena 24 Februari, 1983 hadi pale alipoaga dunia.
Uongozi wa Sokoine ni mfano mkubwa wa kuigwa kwa sababu alivyokuwa na maadili, ufuatiliaji na utendaji kazi makini huku akikemea ulaji rushwa na ubadhilifu wa mali za umma.
Toka miaka ya themanini hadi leo hii Watanzania wengi wako na Edward Moringe Sokoine vifuani mwao utadhani aliwatoka jana. Sokoine anakumbukwa kwa uadilifu wake na umahiri wake katika kutenda kazi. Mfano huu ni wakutufanya tujiulize na sisi pia kwamba ,wewe na mimi baada ya kifo chetu tutakumbukwa kwa lipi? Na je katika taifa zima la Tanzania leo hii kuna mtu wa kufanana nae katika uadilifu na utendaji?
Edward Moringe Sokoine alikuwa mtu wa watu na Watanzania walimjua hivyo. Hakusimama katika majukwaa au kujitangaza katika vyombo vya habari kuwa anafanya mema, la hasha, lakini hata leo vijana wengi ambayo hawakuwepo katika uongozi wake na hata chini za jirani pia wanatambua kwa kusikia kuwa hakika Edward alikuwa mtu mwema na mwenye haki, mchapakazi hodari. Edward alifahamika kuwa mnyenyekevu, mwaminifu, mtiifu na muadilifu wa hali ya juu, na pia alitufanya Watanzania tuishi katika nchi yetu maisha ya amani kamili.
Sokoine hakujiona kama mheshimiwa bali mtumishi wa Uma wa watanzania. Aliishi kindugu na Watanzania, Jamii yetu na ya kimataifa ilimpa na inaendelea kumpa heshima kubwa. Edward Moringe Sokoine alitukuka katika awamu ya kwanza akiwa Waziri Mkuu. Alikuwa na sifa na kipawa kikubwa katika uongozi wake. Alikotokea wengi hatukujua lakin alikamilisha kile walichosema wahenga kwamba: “Ni desturi ya maisha kuwaficha watu wake bora mpaka tokeo kubwa litokee!”.
Alikuwa ni mchapakazi mfano wake nchi hii haijapata kuona. Uadilifu wake haukuwa na chochote cha kumithilisha. Alikuwa mtu mwadilifu kweli kweli katika matendo yake na katika maneno yake.Pia katika kutenda Sokoine alikuwa mtendaji mahiri. Alitenda kwa wakati muafaka na kwa haki siku zote na kwa hilo wote walimwogopa; wema na waovu. Wengine wakasema Sokoine mkali; na sisi wanatemino tunasema kama kuwa kama yeye ni ukali, basi Sokoine alikuwa mtu mkali sana!
Alikuwa msikivu sana kwa shida za wananchi na huruma yake ilikuwa wazi kwa kila mtu kuiona. Aliposema Sokoine watu waliona furaha na alipotenda wakajaa matumaini. Kiongozi wa kweli hana ahadi nyingi.nHutenda badala ya kuahidi na hivyo ndivyo jinsi alivyokuwa yeye. Jina la Sokoine ni alama ya umoja, upendo na mshikamano kwa Watanzania. Mapambano dhidi ya wahujumu uchumi ndiyo yaliyodhihirisha kilele cha umahiri wa kiongozi huyu.
Kiongozi bora hutambulishwa na kazi nzuri aliyoifanya na watu wake humsemea, Sokoine alikuwa ni kiongozi wa kiwango cha juu sana ambaye kila alipokuwa akipita msafara wake ulijaza watu wenye matumaini makubwa sana ya maisha yao kesho na pambazuko la mabadiliko lilikuwa bayana.
Aprili 12, 1984 nyota hii njema, Edward Moringe Sokoine, ilitimiza kazi yake hapa duniani , aliondoka ikiwa bado taifa na wananchi wakimuhitaji sana ; Sokoine aifariki kwa ajali ya gari wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es salaam. Kifo chake kilileta majonzi makubwa kwa Watanzania wengi ambao walikuwa wanamtarajia sana kwa kuwa alifahamika kama mtetezi wa wanyonge na tumaini la kuinua kiwango chao cha maisha nchini. Mwili wa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao Monduli, mkoani Arusha.
Katika kumuenzi zaidi na kutunza heshima ya jina lake Chuo cha Kilimo na Mifugo Morogoro kilipewa jina la "Chuo cha Kilimo cha Sokoine" ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Sokoine.
Edward aliishi kama kama mwale wa moto wa mshumaa akiaangaza wengi na kuwapatia matumaini makubwa sana bila kujali kuchomeka kwake na kuisha taratibu . Japo hatumuoni kwa macho, lakini taa aliyoiwasha Sokoine ingali inawaka na kutumulika hadi leo . Na wote kwa pamoja tukiamua kuenzi mifano aliyoicha Nyota huyu, itakuwa ni ni dira tosha kuleta mabadiliko makubwa sana nchini.
Today we salute you, wewe ni Nyota yetu na mfano bora wa kuigwa, Historia ya maisha yako ni ya kuheshimika na pia umetuachia urithi tosha na fahari ya kupitisha kutoka kizazi hadi kizazi,sisi tujivunia sana wewe na mfano wako ni wa kuigwa, kwa kuwa umetuonyesha kuwa Uongozi bora na unaojali maslahi ya wananchi nchini kote unawezekana kabisa, wewe ni kioo chetu cha Uongozi.
Edward Moringe Sokoine,
Wewe ni fahari ya Tanzania
Januari 22, 2011
MWANAFUNZI aliyeongoza mtihani wa kidato cha mne kitaifa mwaka 2010.
Lucylight alizaliwa Jijini Dar es Salaam, miaka 18 iliyopita. Alisoma Shule ya Msingi St Mary's Tabata na baada ya alihitimu la saba mwaka 2006 alichaguliwa kwenda Shulea ya Sekondari ya Wasichana Tabora lakini aliamua kwenda Marian Girls alikohitimu kidato cha nne mwaka jana.
Taarifa za maendeleo yake zinaonyesha kuwa akiwa kidato cha kwanza alishika nafasi ya tatu, lakini kuanzia kidato cha pili hadi cha nne alikuwa akishika nafasi ya kwanza.
Taarifa za maendeleo yake zinaonyesha kuwa akiwa kidato cha kwanza alishika nafasi ya tatu, lakini kuanzia kidato cha pili hadi cha nne alikuwa akishika nafasi ya kwanza.
Lucylight Mallya (18), amebainika kuwa ni yatima ambaye wazazi wake wote walifariki dunia miaka minne iliyopita.Akizungumza katika mahojiano maalum, akiwa nyumbani kwa baba yake mkubwa kijiji cha Nguruma wilayani Arumeru, binti huyo aliyekuwa akisoma katika Shule ya Sekondari ya Marian, iliyoko Bagamoyo, mkoani Pwani alisema anamshukuru Mungu, walimu na walezi wake kwa kumwezesha kufaulu.
"Sikutegemea kuwa wa kwanza namshukuru sana Mungu, walimu, walezi wangu hasa baba mkubwa na mama na wote walionifikisha hapa ikiwa ni pamoja na wanafunzi wenzangu....," alisema Lucylight.
Lucylighty ambaye ni kwanza kati ya watoto, wanne walioachwa na marehemu wazazi walofariki dunia mwaka 2006 na (2007), alisema malengo yake ni kuwa daktari. Binti huyo alisema wakati anafanya mtihani huo, somo aliloona gumu lilikuwa ni fizikia, lakini anamshukuru Mungu kuwa amefaulu vizuri na kuwa wa kwanza hapa nchini.
"Mimi nilikuwa napenda sana Kemia, Bailojia na Fizikia na nilikuwa nimejiandaa sana hivyo namshukuru Mungu kunisaidia kutimiza ndoto zangu," alisema Lucylighty.
Baba Mkubwa wa Lucy ambaye ndiye anamlea, Dominick Mallya alisema anashukuru Mungu kwa binti yake huyo kuongoza kitaifa. Hata hivyo, Mallya alisema binti huyo amesoma katika mazingira magumu kwasababu hakuwa na fedha za kutosha hivyo alimwomba mmiliki wa shule hiyo, Father Valentine Bayo kumtafutia mfadhili.
"Mamshukuru Father Bayo kwani tangu mtoto huyu akiwa kidato cha pili hadi kumaliza kidato cha nne alikuwa analipiwa na wafadhili,"alisema Mallya. Hata hivyo, aliomba wafadhili wa kumsaidia, ili aweze kuendelea ya masomo ya kidato cha tano hadi sita na chuo kikuu kwasababu yeye (Mallya) hana fedha za kutosha kuwasomesha watoto wote alionao.
“Tungependa kupata tena ufadhili wa Lucylight ili aweze kuendelea na masomo ya juu katika shule ambayo alikuwa akisoma”. CHANZO: MWANANCHI

Pamoja na Lucy tungependa pia kuwapongeza wanafunzi wengine wanafunzi walioshika nafasi bora kitaifa amao ni: Maria –Dorin Shayo wa Shule ya Wasichana ya Marian, Sherryen Mutoka wa Barbro - Johansson, Diana Matabwa na Neema Kafwimi wa Shule ya Wasichana ya St Francis.