Saturday, November 5, 2011

Tano Tano Za Kujipanga Kwa Kazi!

Hatua 5 Za Kujipanga Kwenye Kutafuta Kazi

1. Malengo! Uwe na dira na malengo binafsi, ujue sifa na nguzu zako ili utafute fursa za kuzikuza, fanya utafiti wa mashirika yanayoweza kukufikisha mwenye malengo yako binafsi.

2. Jipange! Andaa wasifu na barua ya maombi ya kazi zinayokuwakilisha vizuri kwa maelezo na muonekano na mpe mtu apitie kutathmini ubora na usahihi wa maelezo na muonekano.

3. Usibahatishe! Tuma sehemu sahihi na kwa mtu sahihi. Tuma kwa mashirika unayoona yanaendana na malengo yako binafsi, tafuta kujua nafasi sahihi kwenye shirika na hata mtu husika atakayepokea maombi ili uandike jina lake kwenye hiyo barua.

4. Rahisisha! Tumia computer na kutuma barua ya maombi kupitia barua pepe (hii ni rahisi zaidi kuliko kutumia sanduku la posta) na uambatanishe wasifu.

5.  Ng'ang'ania! Fuatilia maombi ya kazi baada ya wiking'ang'ania!  kwa njia ya simu, barua pepe ama nenda mwenyewe. Heshimu jibu watakalokupa. Ukiambiwa watakujibu baada ya muda fulani na wiki ikapita baada ya huo muda, watafute tena.




Waajiri Wanatafuta Vitu Gani 5 Vya Msingi Kwenye Usaili?

1. Mtu mwenye dira na malengo binafsi kwasababu ukiwa na dira ama maono na malengo binafsi:

* utakua makini kwenye kuchagua njia na kukufikisha unakotaka kwenda.

* utafanya kiazi kwa mwajiri kwa kiwango kikubwa kutimiza malengo yao na wewe pia kusogea kwenye malengo yako binafsi.

 hata ruka ruka kati ya waajiri ama kazi mbali mbali, mara kwa mara.

2. Mtu mwenye maadili ya uaminifu, ukweli, uwazi, utu, kuhifadhi siri na kulinda wenzake.

3. Mtu mwenye mtazamo wa kumiliki kama mwajiri kwasababu huyu mtu:

* hatakua anafikiri kama mwajiriwa, bali atachukulia kazi kama mmiliki, anayetunza na kukuza malengo ya biashara.

* atajituma zaidi ya nguvu kazi anayodhani inaendana na mshahara wake ama anafanya zaidi ya mchanganuo wa kazi ulivyoandika. Yaani,kama kuna kitu cha kufanya hazingatii nafasi, muda, kipato; anajitoa asilimia mia moja.

* atakua na uepesi na utayari wa kujifunza.

Ni mtu huyu anayejituma kwa kiwango kikubwa ndiyo atakayeongezwa mshahara ama cheo. Lakini yule atakaye fanya kazi yake aliyoandikiwa tu, basi yeye anastahili kulipwa mshahara aliyoingia kwenye mkataba na mwajiri tu. Ukitaka cha ziada, inabidi ujitoe zaidi.

4. Mtu anayetekeleza kwa ustadi, ubunifu, ubora muda ushindani:


* anafanya utafiti kuhakikisha anachofanya ni sahihi, kwa maelezo, muda, ubora, kinahusisha wahusika na kulenga wapasao.

* anaubunifu wa kutatu changamoto na kuwakilisha kazi kutumia sanaa, teknolojia na njia zinazovutia na kushawishi.

* haridhiki kufanya kitu alimradi akimalize, ni mtu wa kuvuka hata viwango vya ubora alivyowekewa kwenye utekelezaji wa kazi.

* anafanya vyote ndani ya muda ama hata kabla ya kufika muda uliopangwa kwa ajili ya kuwasilisha hiyo kazi.

5. Mtu anayejenga mahusiano na mawasiliano mazuri:

* anapenda kujenga mahusiano yenye kukuza heshima, uelewano, utu, suluhisho baini ya watu wa ngazi zote.

* haogopi kumkosoa mtu alimradi inaleta manufaa kwenye mahusiano na kazi na anafanya kwa uutu na kuhifadhi heshima ya wotw wote.

* anaweza kuzungumza ama kuandika kwa kuhusisha, kushawishi, kuwezesha na kuhamasisha watu wasimame kwa manufaa ya shirika lao. Muhimu pia kwa kiingereza.

* anamuonekano mzuri kwa harufu, usafi, mavazi, tabasamu, anavyotembea, anavyoketi na tabia kwa ujumla.


Vitu 5 Vya Kufanya (na Vitu 5 Vya Kutokufanya Kwenye Usaili)


1. Hakiki Maelekezo! Ukiitwa, hakiki tarehe, muda mahali, afisa muhusika na maelezo ya kuleta kwenye usaili. Usiogope kuuliza ukakosea kufuata maelekezo ama ratiba.

2. Jitayarishe! Tayarisha maelezo, fanya mazoezi ya kujibu maswali na mtu mwenye ujuzi ama tafuta maswali kwenye tovitu mbalimbali na muombe mtu akuulize, tayarisha nguo safi za kikazi na heshima za kuvaa, uwe msafi (oga, piga mswaki, safisha kucha).

3. Fika Mapema! Fika nusu saa kabla ya usaili, ujipe nafasi ya kusafisha uso, kurekebisha nguo, kujisafisha makwapa na kupuliza marashi (kiasi), kunywa maji (na kutafuna kitu kutoa harufu mbaya mdomoni (kama utahitaji, lakini hakikisha hakiko mdomoni mnapoanaza mazungumzo)).

4. Salimia Vizuri! Mshike afisa wa usaili mkono ukisalimia  na tabasamu na kumuangalia usoni, halafu uachie mkono wake.

5. Uwe Huru! Weka vitu vyako pembeni, iache mikono yako, na vidole vimeshikana, karibu na mwili wako, ili usitumie mikono sana (usishike kitu mikononi, utakichezea bila kujua ukiwaunaongea), tulia kwenye kiti (usicheze na kiti), uliza usipoelewa, kumbuka kusema "ndiyo, asante, tafadhali".


Vitu 5 Vya Msingi Kwenye Wasifu


1. Itoe maelezo ya malengo yako kwenye fani, elimu, ujuzi, mafanikio yako mpaka sasa na wathibitisha watatu wa maelezo yako ya elimu na ujuzi.

2. Ichapishwe kwenye computer kutumia "Fonts" kama Times New Roman, Arial, Calibri, Cumbria za "Font Size" 12.

3. Iwe na mpango na mtiririko mzuri unaoonyesha tarehe, jina la shirika/shule na mahali uliposoma ama kufanya kazi (nenda www.google.com kutafuta "Curriculum Vitae templates" ama "Curriculum Vitae samples".

4. Isiwe zaidi ya kurasa mbili (na pande mbili tu, siyo kurasa mbili bali kila moja imeandikwa pande mbili mbili)

5. Iwe ya ukweli, watu hua wanafanya utafiti kuthibitisha maelezo yako.


Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Helen Mushi kwenye hmushi@pa.co.tz

No comments:

Post a Comment